Useja mtakatifu
Mandhari


Useja mtakatifu ni aina ya useja ambayo mwanamume au mwanamke anaishika kwa hiari kwa sababu za kidini, hasa katika Ukristo, ambapo lengo ni kuungana zaidi na Yesu aliyeishi hivyo. Ndiye aliyehimiza wanaojaliwa kuelewa uhusiano wa useja na ufalme wa Mungu waushike kweli (Math 19:11-12).
Useja huo, ambao unamdai aliyeushika ajinyime kabisa ndoa na furaha zote za kijinsia, ni msingi wa aina zote za utawa. Pia unadaiwa na Kanisa Katoliki kwa baadhi ya mashemasi na mapadri pamoja na maaskofu wote. Makanisa ya Kiorthodoksi yanaudai kwa maaskofu tu.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- L. Legrand : La Virginité dans la Bible, Paris, Cerf, 1964. (Kifaransa)
| Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |